Page 72

Ndoa ni ya Kudumu

Wiki ya 10 Nguvu ya Vita vya Kiroho

Uumbaji wa Timu ya Mwili Mmoja

Katika bustani ya Edeni, Mungu aliiwezesha timu ya kwanza ya mwili mmoja kupigana vita vya kiroho. Aliwapa wote wawili, mwanamume na mwanamke uwezo kwamba pale wanapoungana, inakuwa timu isiyoweza kushindwa. Kwa bahati mbaya, vita vya mwili mmoja vimelegea sana tangu anguko. Familia nyingi huamini kwamba kama mwenzi mmoja anapigana vita vya kiroho, hiyo hutosha. Kwa bahati mbaya, hiyo ni sawa na kwenda vitani ukiwa umechukua silaha nusu na ngao nusu. Ndiyo maana kuna watu waliouawa vitani.

 

Kama hakuna mmoja wenu aliye shujaa wa kiroho, basi ni muujiza kwamba mpaka sasa bado umesimama kwa miguu yako. Kama timu, ninyi mmewezeshwa kwa ajili ya vita vya kiroho na somo hili litawafundisha ninyi wanandoa jinsi ya kupigana na adui. Kama hupigani na adui kwa pamoja, unapoteza rasilimali muhimu sana.

 

Kama umekuwa ukipigana vita vya kiroho bila kumshirikisha mwenzi wako, huu siyo muda wa kumfundisha mwenzi wako kuwa unajua kiasi gani. Kile mlichojifunza ni sehemu tu ya kile mnachopaswa kukifahamu kwa pamoja. Ruhusu muda huu uwe ni wa Bwana kuwafundisha nyote wawili.

Page 73  © 2=1 ~ Gundua Nguvu

Tuna Uwezo Ule Ule Uliokuwa Ndani ya Adamu na Hawa

Mna uwezo ule ule Mungu aliouweka kwa Adamu na Hawa. Hata hivyo uwezo huo uliathiriwa na anguko.

 

Katika somo la 2 tulijifunza kwamba “msaidizi” hutokana na neno la Kiebrania lenye maana ya “kuzungushia.” Neno lilo hilo “msaidizi,” limetumika mara mbili tu kama “msaidizi wa kufanana naye” na mara zote mbili limetumika kumaanisha mke wa Adamu [Mwanzo 2:18,20].

 

Mara zingine zote neno hilo limetafsiriwa “msaada,” likimrejelea Mungu katika jukumu lake kama msaada kwa Israeli vitani. Mungu hakushuka chini tu na kumwangamiza adui. Badala yake alimpa Israeli mbinu zilizopelekea ushindi. Kuna wakati ambapo Israeli hakuhitaji hata kupigana kutokana na mbinu iliyoletwa ya kumchanganya adui. Katika hali zote, Israeli aliponywa dhidi ya maangamizi makuu kwa msaada wa Bwana.

 

Mungu aliweka uwezo ule ule ndani ya mwanamke ili kusaidia vitani. Tumeiita “rada.” Ni ule ufahamu wa ndani kama kuna tatizo linataka kujitokeza. Ni uwezo wa kutambua kwamba mtoto fulani yuko kwenye shida kabla hata simu haijalia. Ni kile kinachomsukuma mwanamke kuomba kwa ajili ya mumewe aliyeko kazini kabla hajarudi nyumbani na kumweleza kwamba alikuwa na siku ngumu sana. Ulimwengu umeita uwezo huu majina mengi tu. Mungu aliita “msaidizi wa kufanana naye” Adamu. Ni kama “rada” inayochunguza mbali na kuona shughuli za yule adui kwa mbali.

 

Mungu pia aliweka uwezo wa kulandana ndani ya Adamu. Alimfanya kishujaa. Mungu aliweka shauku ya kushinda ndani ya Adamu. Adamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu, alikuwa mzuri sana! Adui alipomkaribia, Adamu aliinuka na kupigana, akitambua kwamba ushindi ni wake. Katika bustani ya Edeni, Shetani alipojifananisha na nyoka, akaingia katika mipaka ambayo hakuwa na kibali cha kuingia, utaratibu wote uliharibika.

 

 

Mbinu ya kwanza ya Shetani ilikuwa ni kuipiga kwanza rada. Hii ni mbinu hata katika vita vya kisasa. Ukiipiga rada, umempofusha mpinzani. Swali lake lilikuwa, “…Ati! Hivi ndivyoalivyosema Mungu…?”

 

[Mwanzo 3:1]. Mbinu yake ilifanya kazi, rada ikashindwa na Hawa akadanganyika [2 Wakorintho 11:3; 1 Timotheo 2:14].

 

Kufuataia kushindwa kwa rada, shujaa alishindwa. Hakuweza kusimama na kumshinda adui. Badala yake, hakumtii Mungu na kula tunda la Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya [Mwanzo 3:6].

 

Mara uwezo huo ndani ya mume na mke vikapotoshwa.

 

Badala ya kunasa siginali za mashambulizi ya adui, sasa rada inanasa mambo ya mwili (hofu, mashaka, upinzani, wasiwasi na fadhaa). Yote yanasomeka kwa uzito ule ule kama ugunduzi wa kiroho. Manung’uniko na chuki, mara nyingi kwa waume zao, ni matokeo ya kuelemewa. Shujaa aliyeumbwa kumshinda adui yake wa kiroho, sasa anapigania ushindi dhidi ya watu wengine. Mashindano na uchoyo yamekuwa mbadala wa ubora wa kiroho. Katika michezo, watu hushindana na watu wengine hata mahali pa kazi. Mara nyingi waume hukata mawasiliano na wake zao hivyo kutosikiliza mashauri yao, hivyo kuwaacha washambuliwe na yule adui.

 

Huu ni muda wa kufufua uwezo huo wa kitauwa katika familia za Kikristo. Mke anapotumika mahali pake kama “rada” huku akizichunguza dalili za yule adui, familia itakuwa haiingiliki kwa mashambulizi ya yule adui.

 

Wanawake, mlipewa uwezo huo wa utambuzi wa ndani. Mungu ndiye aliyeuweka uwezo huo ndani yenu.

 

Wanaume, mlikusudiwa kushinda. Mlikusudiwa kuwa wazuri zaidi ya adui yenu, Shetani. Amka na pigana vita!

 

Uwezo huu utahitaji kunolewa vizuri. Hii itatokea tu kama nyote wawili mtaomba kwa pamoja na kujifunza kutenganisha ya kiroho dhidi ya kimwili. Kadiri mnavyotumia muda mwingi na Roho

wa Mungu, ndivyo itakavyokuwa rahisi kwenu kugundua.

 

Kila mmoja atamhitaji mwenzake ili kuikamilisha kazi. Mume, msaidie mkeo kunoa stadi za rada yake. Omba pamoja naye ili kugundua fadhaa za kimwili na viashiria vya kiroho. Mke msaidie mumeo ili asimame kama shujaa kwa ajili ya familia. Mwite kama kuna shambulizi. Msaidie vitani: usimpinge.

Page 74  © 2=1 ~ Gundua Nguvu

Maingiliano

Je, unaweza kufikiria njia moja adui amepata ufikiaji wa nyumba yako.

Chukua a dakika chache sasa na tujadili hili.

Omba na umwombe Bwana akuonyeshe jinsi ya kufanya kupata ushindi katika eneo hilo.

Ulinzi wa Mungu

Mungu hakutumi vitani bila kuwa na ulinzi. Ametoa silaha  za kuvaliwa [Waefeso 6:11,13-18]. Tunaipokea silaha yetu pale tunapomwamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wetu na kupokea ujazo wa Roho Mtakatifu. Siyo kitu tunachotakiwa kukivaa kila siku. Tunakivaa wakati wote, hata kama ni usiku. Ni muhimu sana, kukumbuka kila siku kwamba umeivaa.

 

Ina maana gani kukumbuka kuvaa silaha yako? Ni ulinzi wako wa kiroho. Kuivaa silaha yako humaanisha kutembea katika ukamilifu wote.

 

Chapeo ya wokovu hufunika akili chetu na hulinda mawazo yetu. Tukiivaa tunaona kwa macho ya Yesu na kusikia kwa masikio ya Yesu.

 

Dirii ya haki hufunika moyo chetu. Maandiko yanasema tuulinde moyo wetu kwa bidii kwa sababu humo hutoka chemchemu za uzima [Mithali 4:23]. Ni hali ya Yesu tu ndiyo inaweza kubadili mioyo yetu.

 

Mshipi wa kweli hufunika viuno chetu. Kiuno ni sehemu zinazotoa uhai katika mwili wetu. Neno ndiyo kweli na tukikaa ndani yake tutatembea katika ukamilifu wa uzima wa milele.

 

Miguu yetu ifungiwe utayari wa Injili ya Amani. Tuna ujumbe muhimu wa kupeleka na mahali pengi pa kuupeleka. Tuwe tayari kwenda kwa amani po pote na wakati wo wote Mungu anapotutuma katika siku nzima. Kwenda hakupaswi kusumbua amani yetu kama tunakwenda kwa kazi ya umisheni kwa ajili ya Bwana.

 

Tunapaswa kuibeba ngao ya imani ili kuizima mishale ya moto ya yule adui. Kama hatukai katika imani, adui atatugandamiza kwa matukio. Tunapaswa kuzuia hofu na mashaka kwa ngao yetu.

 

Chukua upanga wa Roho, ambao ni neno. Tunapaswa kuwa katika neno kila siku. Ni silaha ya mashambulizi lakini pia ni silaha ya kujilinda. Silaha zingine zote ni za kutulinda. Kama tunapenda kuendelea mbele, lazima tuwe tayari kushambulia. Neno ndiyo upanga wetu. Lazima liwe ndani ya mioyo yetu na vinywani mwetu [Kum. 30:14].

 

Hatimaye, omba katika neno bila kukoma. Lazima tupande katika Roho, na siyo katika mwili [Warumi 8:5]. Hii ni kama simu yetu ya kazini. Hutuwezesha kuwa katika mawasiliano muda wote pamoja na Kamanda Mkuu kwa ajili ya maelekezo.

Page 75  © 2=1 ~ Gundua Nguvu

Vifaa Vingine Tulivyopewa kwa Vita

Tuna mamalaka ya jina la Yesu.

 

Kabla ya kupaa kwake Yesu alisema mamlaka yote mbinguni na duniani amepewa yeye

[Mathayo 28:18].

 

Amesema atatenda kila tutakachokiomba kwa jina lake [Yohana 14:13].

 

Ametupa mamlaka kwa jina lake kwamba kile tunachokifunga,[ kuzuia, kubatilisha] na kukifungua hapa duniani kitakuwa kimefunguliwa mbinguni [Mathayo 18:18].

 

Sisi tunaokaa kwake tuna mamlaka ya Jina lipitalo majina yote.

 

Pia ametupa nguvu ya damu yake. Ushindi dhidi ya Shetani ulipatikana kwa kumwagika damu ya Yesu [Waebrania 9:22,26; Ufunuo 12:11]. Mara tunapompokea yesu kuwa Bwana na Mwokozi, nguvu ya damu yake hutenda kazi maishani mwetu. Damu ya Yesu ilimwagika kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu, siyo kwa ajili ya vitu au wanyama. Kwa sababu ni washirika wa agano na Mungu, tunao ulinzi wa Bwana kwa vitu tunavyomiliki. Ayubu 1:10 huzungumzi ukigo wa ulinzi anaouweka Mungu kwa watu walio na agano naye. Katika Yohana 17:11, Yesu alimwomba Baba atulinde. Tunaweza kuuita ulinzi huo kwa ajili ya wanyama wetu na mali zetu wakati wo wote kwa jina la Yesu.

 

Pia tumepewa nguvu  ya  sifa. Bwaba    huziishi  sifa ya watu wake [Zaburi 22:3] na ameweka wakfu sifa ili kumnyamazisha adui [Zaburi 8:2]. Msifu Mungu mara kwa mara katika muda wako wa maombi na kwa siku nzima. Ni silaha yenye nguvu sana na yeye anastahili sifa.

 

Kuhusiana na silaha, tunamzidi adui. Ingawa tu binadamu, hatupigani kwa silaha kibinadamu. “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu ahata

kuangusha ngome); tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia” [2 Wakorintho 10:4-6].

 

Silaha alizotupa Mungu ameziwezesha mwenyewe. Kwa asili zina nguvu ya ajabu [Kum. 33:27, Zekaria 4:6]. Tunaweza kumshinda adui maana yeye alimshinda [Yohana 16:33, 1 Yohana 4:4; Warumi 16:20]. Ushindi wetu hautegemei uwezo wetu wenyewe.

 

Ingawa majeshi ya adui hufanya vita na watakatifu [Ufunuo 19:19] na ni kwa ajili ya kutuangamiza [Yohana 10:10], silaha zao ni ukomo. “Jaribu halikuwapa ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ani mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili” [1 Wakorintho 10:13 ].

 

Andiko hili linatuthibitishia kwamba silaha za adui ni za mwili [za kawaida kwa mwanadamu], zina nguvu yenye kikomo, na kwa kila shambulizi tumehakikishiwa kuna mlango wa kutokea kama tutamtegemea Bwana.

 

Silaha za adui huwa na mvuto kwa mwili [Warumi 8:5,6; Gal. 5:19-21 na 6:8]. Silaha zake huleta ugomvi na mafarakano [Yakobo 3:16 na 4:1-3]. Kaa katika roho wakati ukipigana na yule adui. Silaha zetu zina nguvu zaidi na daima tutamshinda tukikaa katika roho. Kama tutakaa katika mwili, hakika tutashindwa na yule adui. Yeye ana uzoefu mkubwa zaidi yetu juu ya mwili.

 

Kama silaha zetu zina nguvu kuliko zile za adui, kwa nini sasa tunaanguka katika mashambulizi ya adui?

 

Tunapaswa kuwa makini. 1 Petro 5:8 inasema, “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshtaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye , huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.” Kama mwili mmoja wa wanandoa, tunapaswa kukagua ukigo wetu kila siku [Ayubu 1:10]. Ona kama kuna mashimo au nyufa zinazoweza kumwingiza adui. Jali onya la Mithali 27:23, “Fanya bidii kujua hali ya makundi yako, na kuwaangalia sana ng’ombe wako.”

 

Je, huwa unamtafuta Bwana kila siku kwa ajili ya mwenzi wako na watoto wenu? Je, unamwomba Mungu ii akupe ugunduzi wa shughuli za yule adui? Mume na mke wapate muda maalum kwa wiki ili kufunika shughuli zote binafsi na zile za kifamilia. Wewe, rada, huika, na wewe shujaa, kesha.

 

Kuna aina mbili za vita tunavyopaswa kuvipiga, vya kujilinda na vya kushambulia. Uko kwenye hali ya kujilinda kama adui tayari amekwisha kukushambulia. Tumia silaha ambazo Mungu amekupa ili kumwondoa adui na kuirejesha mipaka. Hii ni ya kuzingatia sana. Tumewahi kusikia ikisemwa, “ Kusudi la vita siyo kusalimika, ni umiliki.” Hata vita vyetu vya kujilinda vinapaswa kudai mipaka irejeshwe.

Ni  muhimu  kujifunza  kuvipiga  vita  vya  kushambulia.  “waipeleleze  nchi”  iliyoko  mbele yenu [Hesabu 13:17]. Usiombe tu kwa ajili ya leo, endelea katika maombi ukifunika mamboyajayo. Kwa mfano, je, un aombea ulinza wa watoto wako? Je, unaombea miamala ya shughuli zenu?

Usisubiri mpaka uwe katikati ya tatizo ndipo uombe unavyoona. Tafuta ushauri wa Mungu kabla hujafikia hatua hiyo.

 

Vita vya kujihami huwa ni rahisi kuvipiga. Utakuwa umenyanyua mkono juu wakati ukitoa dua ili kutambua mipango ijayo ya adui. Jifunze zijaribu roho.“Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zinatokana na Mungu” [1 Yohana 4:1].

 

Tumepewa uwezo wa kiroho ili kumgundua adui. Shetani na majeshi yake wana mbinu za werevu na mara nyingi hutushawishi kwamba adui ni mwenzi wetu, watoto wetu, mkuu wetu kazini, au ndugu zetu katika Kristo. Hii hutufanya tupigane sisi kwa sisi hivyo kumpa adui uhuru wa kutawala maisha yetu.

 

Tunapopigana na adui, mara nyingi “tunalipua tu” maombi yetu wakati tulitakiwa kwanza tupate mahali pa kupiga ndipo tulenge hapo. Waefeso 6:12 inachambua vizuri sana na kupambanua majeshi ya adui kwa ajili yetu.

 

Kwanza “falme” kutokana na neno la Kiyunani “arche,” lenye maana ya “daraja la juu” la kiutawala. Haya ni majeshi ya kiwango cha juu kabisa ya adui.

 

Kifuatacho ni “mamlaka,” hutokana na neno la Kiyunani “exousia,” maana yake “mamalaka iliyoteuliwa” au “himaya.” Yana milki sehemu fulani ya dunia.

 

Kisha tuna “wakuu” kutoka kwenye neno la Kiyunani “kosmokrator” au “mkuu wa ulimwenfu huu.” Haya ni mapepo yaliyotumwa kuwaongoza watawala wa ulimwengu huu.

 

Hatimaye, “uovu wa kiroho,” kutokana na neno la Kiyunani “poneria,” kumaanisha “uasi,” ni daraja la chini, lakini ndilo kubwa katika majeshi ya Shetani.

 

Ukiwa katika vita vya kiroho, mwombe Roho Mtakatifu akupe ugunduzi. Je, unapigana dhidi ya uovu wa kiroho au dhidi ya falme na mamlaka?

 

Mara nyingi tunapogigana vita huwa tunafikiria kwamba inaathiri familia yetu tu lakini ukweli ni kwamba ni roho inayotawala nchi yetu au sehemu ya nchi na inaathiri familia zote zinazotuzunguka.

 

Anza kuwa na jambo maalum katika maombi yako. Mwombe Roho Mtakatifu apadhihirishe pale unapopaswa kulenga ili kwamba uelekeze kwenye lengo.

 

Anza kuvikaribia vita vya kiroho mkiwa kama timu ya mwili mmoja. Nguvu yenu ni huongezeka  na mtokeo hupatikana kwa haraka sana. Msimruhusu Shetani awatawanye ninyi wawili.

 

Umoja wenu ni ufunguo kwa mafanikio yenu katika vita vya kiroho kwa ajili ya familia na nyumba yenu. Mwombe Roho Mtakatifu aanze kuwafundisha kuendana kwa pamoja katika vita. Kumbukeni, nguvu

yenu imegawanyika kwa usawa kadiri mnavyotenda kazi kwa pamoja [Law. 26:8]. Matokeo utakayoyapata yana thamani kwa muda na nguvu iliyotumika kugundua nguvu zinazoendana katika vita vya kiroho.

Page 76  © 2=1 ~ Gundua Nguvu

MAELEZO YA MAJADILIANO

© 2=1 ~ Gundua Nguvu

Nguvu ya Vita vya Kiroho Kikao cha 10

Shiriki na kila mmoja eneo moja ambalo umeona adui akivamia maisha yako huko nyuma.

 

Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za shetani. Waefeso 6:10-11

Kabla ya andiko hili Paulo ametoa maagizo kwa watoto na wazazi, watumwa na mabwana. Inaonekana anazungumza na wale walio na mamlaka na wale ambao wanapaswa kujibu kwa mamlaka. Unafikiri ni kwa nini anaendeleza mjadala wa silaha za Mungu kwa maagizo hayo?

Paulo anatupa sababu gani ya kuvaa silaha zote za Mungu?

Ujanja wa shetani ni nini?

Shirikianeni eneo lingine ambalo mmemuona adui akija kinyume na ndoa yenu siku za nyuma.

 

Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Waefeso 6:12

Watu sio shida yetu. Nini?

Unafikiri hoja ya Paulo ni nini katika kuainisha viwango mbalimbali vya upinzani wa adui?

Katika kujifunza kumtambua adui, kwa nini unadhani ni muhimu kujua unapambana na kiwango gani?

Shiriki na kila mmoja jaribio ambalo unaona na adui kuharibu uhusiano wako sasa!

 

Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho… Waefeso 6:14-18

Shiriki na kila mmoja jambo lolote jipya ulilojifunza kutoka kwa kipindi hiki kuhusu kila moja ya sehemu hizi za silaha.

(1) Bamba la kifua la haki

(2) Miguu kufungiwa Injili ya amani

(3) Ngao ya imani

(4) Chapeo ya wokovu

(5) Upanga wa Roho

(6) Mkanda wa ukweli

Unafikiri ni kwa nini imani huzima mishale yenye moto ya adui?

Kwa nini unafikiri unapaswa kuwa “kuomba daima”. Usisahau kwamba kuomba pamoja huongeza uwezo wako wa vita vya kiroho!

 

Amin, amin, nawaambia, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba yangu. Yohana 14:12-14

Je, unaamini kwamba inawezekana kufanya mambo makubwa zaidi ya Yesu?

 Ikiwa ndivyo, hilo linawezekanaje?

Tumezungumza hapo awali kuhusu Yesu kufanya mapenzi ya Baba yake tu. Je, ninyi nyote wawili mnawezaje kutafuta mapenzi ya Baba ya kufanya mambo makubwa kuliko Yesu alivyofanya?

Shirikiana jinsi ambavyo ungependa iwe wakati unafanya mambo makubwa kuliko Yesu.

Shiriki “milango iliyo wazi” yoyote ambayo unaweza kuona ambayo inakupa ufikiaji wa adui nyumbani kwako.

Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome, tukiangusha mabishano na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo, na kuwa tayari kuadhibu. kutotii wakati utiifu wako umetimia. 2 Wakorintho 10:4-6

Silaha zako ni za kimbinguni – si za kawaida, za kibinadamu. Je, hii inakuambia nini kuhusu nia ya Mungu kwako wewe kuwa mshindi katika vita vya kiroho?

Angalia maelezo ya silaha zako hufanya nini na uongee kwa nini hizo ni muhimu katika vita.

Shirikiana jinsi unavyoona rada na shujaa wakifanya kazi pamoja na silaha hizi.

Shiriki na kila mmoja jinsi ungependa kuwaona nyinyi wawili mkikabiliana na changamoto zozote za sasa za adui.

 

Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; lakini Mungu ni mwaminifu ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo, lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. 1 Wakorintho 10:13

Silaha zetu ni za ajabu, lakini adui anaweza tu kutumia silaha ambazo ni za kawaida kwa mwanadamu – silaha za asili, za kimwili.

Kwa nini ni muhimu sana ukae katika roho unapompinga adui?

Adui amekuwa na karne nyingi kutazama tabia za wanadamu.

Unafikiri kwa nini anataka kukuweka umakini katika mwili?

Je, unafikiri Mungu hutoa njia gani za kutoroka unapojaribiwa?

Shiriki leo na kila mmoja hali ambapo ulishinda jaribio la adui kuvamia maisha yako.

 

Hayo nimewaambia, ili mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mtakuwa na dhiki; lakini jipeni moyo, mimi nimeushinda ulimwengu. Yohana 16:33

Ijapokuwa uko vitani na adui, Yesu anataka uwe na amani. Je, unaonaje katika maisha yako kwamba Yesu ameushinda ulimwengu?

Je, kuna uwiano gani kati ya kupigana na mashambulizi ya adui na kupumzika kwa amani ndani ya Yesu?

Unahitaji kufanya nini ili kufanya kazi pamoja kama rada na shujaa?

© 2=1 ~ Gundua Nguvu

Translate »
error: Content is protected !!